Ijumaa, 5 Septemba 2014

Gardner G Habash Azungumzia Tetesi za Kuachana na Lady Jay Dee


Gardner G Habash Azungumzia Tetesi za Kuachana na Lady Jay Dee na Chanzo Chake, 'Hatuna Tatizo'Gardner G Habash Azungumzia Tetesi za Kuachana na Lady Jay Dee na Chanzo Chake, 'Hatuna Tatizo'
Gardner G Habash amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kwenye mitandao kuwa yeye na mkewe Lady Jay Dee wako kwenye wakati mgumu wa ndoa yao. Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo ni taarifa zisizo za …

Alhamisi, 17 Julai 2014

Timaya wa Nigeria asema alitumia zaidi ya milioni 200 kukamilisha collabo na Sean Paul.

Timaya wa Nigeria asema alitumia zaidi ya milioni 200 kukamilisha collabo na Sean Paul


Msanii wa Nigeria, Timaya ameeleza kuwa alitumia zaidi ya N20m (zaidi ya milioni 200 za Tanzania) kukamilisha collabo aliyofanya na Sean Paul katika remix ya wimbo wake ‘Bum Bum’.
Msanii huyo amesema kiasi hicho cha pesa kilitumika katika kutengeneza audi na video ya wimbo huo.
Pamoja na kutumia kiasi hicho cha pesa, ilimchukua miezi 6 ya mipango hadi kukamilisha zoezi zima.
 “Nilitumia zaidi ya N20m katika wimbo huo na video. Ilinicost kiasi hicho kumleta Sean Paul na watu wake kutoka Jamaica, sitanii.” Timaya aliiambia Toolz.
Posted by

Warembo Mmeipata Hii,Kope za bandia zinaweza kusababisha upofu.

Warembo: Kope za bandia zinaweza kusababisha upofu

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia.
 
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa.
Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi.
Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.
Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’. Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae.
Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi.
Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.
Posted by