Jumapili, 29 Desemba 2013

JACK PATRICK ADAIWA KUNASWA NA PIPI 66 ZA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA MIL 215.5 CHINA

Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
Mwanamitindo Jack Patrick.…
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick akipelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya mkutano na wanahabari Jumanne Desemba 19, 2013 huko Macao China.
Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick.
Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa hizo za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
MODO maarufu Bongo, Jacqueline Patrick Cliff, anadaiwa kukamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao nchini China. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya pipi 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Jack alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Jack alipata jina aliposhika namba tatu kwenye Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia uliuza nyago kwenye video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marehemu Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain. Kuanzia hapo jina likawa kubwa na akawa mwanamitindo maarufu Bongo.
Ni katika kipindi hicho cha umaarufu akaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar akikabiliwa na msala wa

MWANA MZIKI P CAT ATAACHIA WIMBO WAKE MPYA MKOANI D'SALAAM


mwana mziki P CAT akiwa katika pozi jijini dar


Mwana mziki huyu atachia wimbo wake mpya kwa jina la  SWING,swing maana yake HOBI,au kitu mtu ancho pendelea kufanya mwanamziki huyo alisema "napenda kuwaambia mashabiki wangu na watu wote,fanya unachopenda, nami napenda mziki" kwa mujibu wa chanzo cha habari kimesema kua mwana mziki huyo ataachia Wimbo yake hiyo jijini Dar katika studio mbalimbali za radio kama vile MAGIC FM,TIMES FM CHOICE FM nanyingine nyingi msanii huyo ameongeza kuwa anawahidi mashabiki wake hatawangusha katika wimbo wenyewe na video yake itakua poa sana,
  kwa mujibu wa maneja wake MR Abdul m Abdallah  amesema  kama kuna mtu anatakumtumia msanii huyo anaruhusiwa kwa kuwa yuko huru kufanya kazi na mtu yeyote na anaweza kumtafuta kwa namba 0752041148/0687279136

THE FETTY GIRL