Watoto wa Will na Jada Smith, Willow na Jaden wana mengi ya ndani ambayo wengi walikuwa hawayafahamu. Kwa mujibu wa US Weekly, Willow Smith mwenye umri wa miaka 13 hulala
na nyoka kumi chumbani kwake na baadhi yao hawajafungwa kabisa! Lakini sio pekee ambaye ana mapenzi na nyoka hao, kaka yake Jaden pia
huwachukulia nyoka wa dada yake kama wapenzi wake kwa kuwa huwa
wanaingia chumbani kwake na kulala nae kitandani huku wakijizungusha
mwilini kwake! Willow ameshawazoea nyoka hao kwa kuwa alianza kuishi na nyoka wa kwanza mwaka 2008 wakati akiwa na umri wa miaka 7 tu. Jada Pinkett aliwahi kuliambia jarida la Rebok mwaka jana kuwa yeye
anawapenda sana nyoka na mwanae Willow pia amekuwa anawapenda daima. “Anaweza kwenda kwenye store ya nyoka akachukua nyoka mmoja na
akajizungushia. Sikuwahi kumgusa nyoka hapo kabla, na nilikuwa siwezi
kuwashika…..nimekuwa nampenda Willow daima tangu mwanzo. Nilimwambia
Willow, ‘umemfanyia mama msaada mkubwa. Umenisaidia kushinda uoga’..”
Hakuna asiyejua kwamba Millard Ayo ni Mtangazaji (Clouds
Fm) anayependwa sana siku hizi kwa kukiboresha na kukipamba kipindi
chake kinachokwenda kwa jina la "AMPLIFAYA" huku mwenyewe akijiita "MR.
COUNT DOWN" ambapo huwa anatoa stori kumi za moto kila siku. Mtangazaji huyo anawania vipengele tofauti vya Tuzo za Watu na ni matumaini ya wengi jamaa atanyakua Tuzo hizo. Hivi karibuni Wema Sepetu amempigia debe
au kwa maneno mengine amewashawishi mashabiki zake kumpigia kura zaidi
Millard Ayo ili aweze kuibuka kidedea katika kura hizo. Bila kisilani
chochote Millard Ayo alisoma hewani ujumbe huo katika kipindi chake
ikiwa ni moja ya kipengere ndani ya kipindi chake ambacho kinahusisha
kuzirusha jumbe mbalimbali alizotumiwa kupitia mitandao yake ya kijamii,
na moja ya ujumbe aliousoma na kushukuru sana ni kutoka kwa mrembo huyu
wa
Mwimbaji wa kike wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23
anaefahamika kwa jina la Adokiye ameeleza anachofikiria kuhusu wasichana
zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram. Mwimbaji huyo ambaye anafahamika sana kwa comments za zinazotengeneza mijadala hudai kuwa yeye ni bikira. Mwisoni mwa wiki hii ameiambia Showtime kuwa anajitoa yeye kwa kundi
la Boko Haram kama inawezekana wao kuwaachia wasichana wanaoshikiliwa na
kundi hilo. “Sasa hivi ni saa tanto usiku, je unajua ninachofikiria? Wale
wasichana wadogo, wapi walipo na nini kinawatokea muda huu. Sio sawa. Ni
wadogo sana. Nawishi ningeweza kujitoa mimi kubadilishana nao. Wana
umri kati ya miaka 12 hadi 15. Mimi ni mkubwa na nimeshazoea maisha
zaidi yao. Hata kama wanaume 10 hadi kumi na mbili watanichukua kwa
usiku mmoja, sijali. Nachojali waachie hao wasichana warudi kwa wazazi
wao.”