Jumatano, 15 Januari 2014
Picha, Profesa Jay Na Diamond Wakiwa Bongo Records, Soma Alichoandika Jay.
Nikki Mbishi Anafanya Kitu Tofauti Kwenye Huu Wimbo
Rapper anayeaminika kuwa na uwezo mkubwa wa mitindo huru na mistari ya nguvu kwenye kazi zake za muziki ameweka post ya picha kuhusu his next big collabo itakayo husisha msanii kutoka Kenya na Mwingine kutoka Tanzania.
Sauti ya King Wa Rapper Kutoka Kenya Collo Na Msanii/Mtangazaji Vanessa Mdee zitasikika kwenye wimbo huo. Utaitwa Toast Of Life.
Pole Kwa Msanii Rich Mavoko Kwa Kumpoteza Baba Yake Mzazi
Kijana mwenzetu Richard Martin Maarufu Kama Rich Mavoko leo amempoteza Baba Yake Mzazi Mr Martin.
Taarifa zaidi nimezipata kutoka kwa Aliyekuwa manager wa Rich Mavoko, ameiambia sammisago.com kuwa Baba yake anaishi Morogoro na mara nyingi Rich husafiri kwennda kumuona anapokuwa anaumwa.
Rich Mavoko ameandika ameandika hivi kwenye acccount yake ya instagram “R.I.P my Father… amefariki sasa ivi jamaniiii….” post iliyowekwa na picha ya giza.
ANGALIA ZAIDI YA WATU 200 WALIOZAMA KWENYE MTO NILE WAKIKIMBIA VITA

Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti
kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.
Boti hiyo ilizama ikiwa imewabeba watu wengi kupita kiasi kinachotakiwa kwa uwezo wake.
Watu hao walikuwa wanakimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Mapigano yalianza Sudan Kusini mwezi December mwaka jana baada ya
Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar kwa
kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)