Jumanne, 12 Novemba 2013

WEMA NA PENNY WAFIKIA MUAFAKA WA PENZI LA DIAMOND.ADAI YUKO TAYARI KUCHANGIA PENZI.


Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bon- go Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia map- enzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayem- penda.


Peniela Mwingilwa ‘Penny’.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, amesema maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhu- siano wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.“Ninampenda Diamond na sitaki kum- poteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha.

Kama Diamond anaona kuna msicha- na mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.

Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006.

HICHI NDICHOO KISA KILICHO MFANYA JACQUELINE WOLPER KUBADILI DINI


Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa
wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabik zangu stak maswal nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

HATIMAYE DIAMOND ACHAGUA MREMBO WA KUMUOA KATI WEMA AU PENNY, SOMA HAPA...!

Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.

Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.

Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.

“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.

Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”

Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.

“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:

Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.

Juzi Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Penny ili kutaka kupata maoni yake kuhusu tamko la Diamond, lakini muda mrefu simu hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Baada ya kumkosa Penny, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Wema, naye kama Penny, simu yake iliita mara kadhaa lakini haikupokelewa.

Tazama Mjengo Mpya(Nyumba) Anayojenga Diamond Platnum na Kusababisha Jana Usiku Mjadala Mkubwa

Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi.


Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.

''Toa kitu weka kitu...! Ndio tulivyo funzwa...stareh tunawaachia wajanja wa mji...

Haijajulikana mjengo huu uko maeneo gani wala umegharimu kiasi gani ila inaendelea kudhihirisha mafanikio anayoendelea kuyapata Diamond.