Tuma neno PERUZI kwenda 15368 kupata habari za bongo Movies sasa. Wateja wa Vodacom Pekee
“Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo
na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani, ameacha kabisa
kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani
alisikiliza ushauri niliompa kabla.”
Hiyo ni kauli ya staa aliyetikisa mwaka 2013 bwana Diamond
Platnumz aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti maarufu
la michezo nchini hivi karibuni.
Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye
katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na
Wema ipo mbioni kutimia.
“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na
Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu
kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo
wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si
kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba
anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu
yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.” Alisisitiza Diamond
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni