Karibu
ndani ya BongoCelebrity. Shukrani kwa kututembelea.Hii ni tovuti/blog
ambayo inaandika kuhusu watu mashuhuri au maarufu wa Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla. Tunaandika na kukupa wewe msomaji nafasi ya
kujadili habari za watu mashuhuri wa zamani na wa sasa hivi. Nia ya
msingi ni kujenga na sio kubomoa.
Tupende tusipende,
maisha ya watu maarufu (celebrities) yana mvuto mkubwa kwa jamii.Iwe ni
mwanasiasa, mwanamuziki,msakata kabumbu,mchekeshaji,mcheza sinema,mpiga
simu maarufu redioni,msanii wa ngoma za asili,za kisasa,mtangazaji
maarufu wa tv au redio,mtu mwenye umbo la aina yake,balozi nk wote kwa
pamoja huwa ni wenye mvuto achilia mbali ushawishi fulani katika jamii.
Inasemekana jamii isiyo na watu wake mashuhuri, maarufu,alwatani nk ni
kama jamii isiyo hai.Tukisikia habari zao huwa mara nyingi tunataka
kujua zaidi.Haina maana kwamba hatuna mambo mengine muhimu zaidi ya
kufanya,la hasha.Ni hulka ya ubinadamu tu. Isitoshe, jamii inaweza
kujifunza mengi sana kupitia mwangaza wa maisha na mienendo ya watu
maarufu/ mashuhuri/celebrities.
Kwa kuzingatia
sababu tulizozitaja hapo juu ndio maana tumejikita katika kuandika
habari za watu hao maarufu. Hapa ndio chanzo cha habari motomoto,
mahojiano, habari za kina, matoleo mapya ya albamu za muziki, picha
kutoka kwa wapiga picha wetu maarufu za matukio, mikasa nk, habari za
chochote kile kipya au cha zamani ambacho tusingependa kisahaulike ndani
ya jamii yetu nk.
Isitoshe hapa ndipo
vipaji vipya vinapotambulishwa, celebrities wapya wanapoanzia. Kwa
maana hiyo ukikuta amewekwa mtu ambaye unadhani bado hana hadhi ya
ki-celebrity usishangae,ndio anaanza safari yake.
Kwa kuzingatia
ukweli kwamba lugha maarufu zaidi ulimwenguni inabakia kuwa kiingereza,
BongoCelebrity inatumia kiingereza na kiswahili kama lugha zake
maalumu.Tunaamini ni muhimu na pia ni jukumu letu, kuienzi, kuiendeleza
na kuikuza lugha yetu ya Kiswahili. Lakini kwa namna yoyote ile
Kiswahili ndicho kinapewa kipaumbele zaidi.
Kama una habari za
mtu maarufu au wewe mwenyewe ni mtu maarufu na unalo jambo ambalo
ungependa liwafikie watanzania na wa-Afrika Mashariki kwa ujumla kupitia
tovuti/blog hii,usisite kuwasiliana nasi kwa kupitia; bongocelebrity at gmail.com au info (at) bongocelebrity.com.Unaweza pia kutumia fomu iliyopo hapo chini.
Maoni ya aina zote
yanakaribishwa ingawa matumizi ya lugha chafu hatuyavumilii. Yawezekana
kabisa kutoa mchango wako au maoni yako bila kutumia lugha zenye matusi.
Pia tunakaribisha matangazo.Kwa
maulizo ya bei au gharama za kutangaza biashara au matukio wasiliana
nasi pia kwa kutumia fomu hiyo hiyo hapo chini.Mnakaribishwa!
Karibuni sana.
Jeff Msangi(pichani)-Mhariri Mkuu
&
BongoCelebrity Team.
Be Sociable, Share!