Jumanne, 5 Novemba 2013

Mama Diamond amkataa WEMA SEPETU..


Image


MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.

Habari za CHUMBANI zimetonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema Sepetu kutokana na tabia zake na kudai kuwa Penny ndo chaguo halali la Diamond.

Akizungumza na gpl nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, mama huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.

“Kuhusu Nasibu kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa msimamo wangu,” alisema mama huyo.

Mwandishi huyo kadiri alivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.

“Hayo ni maisha yake mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni