
Muigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o ametwaa tuzo yake ya kwanza ya Hollywood Film Awards zilizofanyika huko Beverly Hilton jijini Los Angeles, Marekani.

Lupita Nyong’o akitoa shukrani
Nyong’o ameshinda tuzo New Hollywood Award kwa kuigiza filamu ya ’12 Years A Slave’ iliyoanza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema Marekani na Uingereza wikiendi iliyopita.
Pamoja na hivyo, Nyong’o amekuwa akitajwa miongoni mwa waigizaji wanaoweza kuwania kipengele muigizaji bora msaidizi wa kike kwenye tuzo Oscar.

Lupita alijikuta akibubujikwa na machozi ya furaha wakati akitoa maneno yake ya shukrani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni